Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR imeanza kuwarejesha nyumbani kwa hiyari wakimbizi wa Ivory Coast

UNHCR imeanza kuwarejesha nyumbani kwa hiyari wakimbizi wa Ivory Coast

Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR , leo asubuhi limeanza kuwarejesha kwa hiyari nyumbani , maelfu ya wakimbizi wa Ivory Coast kutoka nchini Liberia.

Kwa mujibu wa shirika hilo kurejea kwa wakimbizi hao kumeingiliwa kwa mwaka mzima na mlipuko wa Ebola.

Wakimbizi 11,000 kati ya 38,000 raia wa Ivory Coast waishio katika makambi nchini Liberia wameelezea nia yao ya kutaka kurejea nyumani mara moja, kama anavyofafanua msemaji wa UNHCR Adrian Edward.

(SAUTI YA ADRIAN EDWARD)

"UNHCR inasaidia wakimbizi pindi tu wanapowasili na pia inasaidia katika ujumuishwaji katika jamii nyumbani. Kadhalika kuna programu za kujipatia kipato. takriban watu 300,000 walikimbia machafuko kufuatia uchaguzi wa urais mnamo Novemba 2010 nchini Cote D'Ivoire wakiwemo wakimbizi 200,000 waliokimbilia Liberia. Kurudi kwa hiari kwa wakimbizi hao kulianza mwaka 2012."