Ujumbe mbadala wahitajika dhidi ya itikadi kali kwenye mitandao ya kijamii,

Ujumbe mbadala wahitajika dhidi ya itikadi kali kwenye mitandao ya kijamii,

Leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani kumefanyika mkutano maalum wa kamati ya Baraza la Usalama ya Kupambana na Ugaidi ili kujadili kuhusu jinsi ya kukabiliana na vikundi vya kigaidi vinavyosambaza ujumbe wao kupitia mitandao ya kijamii.

Akihutubia kikao hicho, mwakilishi wa mtandao wa kijamii wa Facebook Monika Bickert amesema suluhu siyo tu kufunga akaunti za magaidi lakini pia kushiriana na asasi za jamii ili kusambaza ujumbe unaopinga maudhui ya ugaidi na kuwezesha vijana kujenga mustakabali wenye stahamala zaidi.

Akizungumza na redio ya Umoja wa Mataifa Monika Bickert amesema umuhimu kwa Facebook ni kuhakikishia siri za watu zinahifadhiwa lakini vile vile usalama wa jamii nzima inayotembelea mtandao huo, na hivyo :

(Sauti ya Bi Bickert)

«  la Msingi kwetu ni uwazi na udhibiti. Tunaangalia kwa makini ujumbe wote unaoweza kuhatarisha watu, ikiwemo ugaidi. Kwa hiyo, kila mara mtu akiripoti kitu ambacho kinahusiana na ugaidi au kinachoweza kuhatarisha maisha ya watu,kinafika kwenye mstari wa mbele wa ufutaliaji wetu na tunahakikisha tunaiangazia mara moja . »