Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uhamiaji na masahibu ya ughaibuni #iammigrant

Uhamiaji na masahibu ya ughaibuni #iammigrant

Tarehe 18 Disemba ni siku ya wahamiaji duniani. Maadhimisho hayo yanafanyika huku mwaka 2015 ukisalia kukumbukwa kuwa mwaka wa machungu ya binadamu na majanga ya wahamiaji. Hii ni kutokana na taarifa kwamba mwaka 2015 pekee zaidi ya watu 5000 wanawake kwa wanaume pamoja na watoto walipoteza maisha yao wakiwa safarini kusaka maisha bora au kuokoa maisha yao. Wengine wengi wanasalia katika mikono ya watu wasio na nia njema wakiwatumia kwa kazi zisizo halali. Je wahamiaji wenyewe wanasemaje? Wakiwa ughaibuni wanakumbwa na nini? Ungana na Joshua Mmali kwenye makala hii ikimgusia mwanamuziki nyota wa Burundi Khadija Nin ambaye naye pia ni mhamiaji.