Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Miaka 10 ya CERF imekuwa ya ukombozi: Ban

Miaka 10 ya CERF imekuwa ya ukombozi: Ban

Mfuko wa dharura wa Umoja wa Mataifa, CERF umekuwa mkombozi kwa waathiriwa wa majanga, amesema Katibu Mkuu wa umoja huo, Ban Ki-moon jijini New York, Marekani katika tukio la kuadhimisha miaka 10 tangu kuanzishwa kwa mfuko huo. Joseph Msami na taarifa zaidi.

(Taarifa ya Msami)

Nats..

Mkutano ulianza kwa onyesho la filamu ya miaka 10 ya CERF ikiwa na sauti ya Kofi Annan, Katibu Mkuu wakati huo akitangaza kuzinduliwa kwa mfuko huo kwa lengo la kuleta ahueni kwa jamii..

Baada ya filamu, Katibu Mkuu wa sasa Ban akatolefa mfano CERF ilivyoleta nuru kwa wahanga wa majanga ya asili huko Nepal, Ethiopia na hata Malawi.

Hata hivyo amesema changamoto zinaongezeka na licha ya ukarimu wa wahisani kuchangia CERF, pesa haitoshi hivyo ameibua michakato miwili, Mosi ..

(Sauti ya Ban)

Jopo langu la ngazi ya juu kuhusu usaidizi wa kibinadamu punde litapendekeza mbinu za kubadili uchangiaji fedha wa uhakika, salama , wa kutosha na unaotabirika kwa ajili ya watu wanaokumbwa na majanga na pili uchangiaji majanga utakuwa kipaumbele wakati wa mkutano wa dunia kuhusu usaidizi wa kibinadamu utakaofanyika Istanbul mwezi Mei mwakani.”

Hata hivyo amesema wakati michakato hiyo ikisubiriwa, CERF inasalia na umuhimu mkubwa katika kukabilia changamoto za sasa za kusaidia wahitaji wa misaada.

.