Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakulima wadowadogo wanakabiliwa na changamoto nyingi:UNCTAD

Wakulima wadowadogo wanakabiliwa na changamoto nyingi:UNCTAD

Shirika la Umoja wa Mataifa la biashara na maendeleo UNCTAD limetoa ripoti ya bidhaa na maendeleo kwa mwaka 2015 na kusema wakulima wadogiowadogo ndio asilimia kubwa ya watu wasikini , licha ya kwamba ndio wazalishaji wa Zaidi ya asilimi 80 ya cha chakula duniani.Grace Kaneiya na taarofa kamili.

(Taarifa ya Grace)

Ripoti inaainisha baadhi ya changamoto wanazokabiliana nazo wakulima hao katika nchi zinazoendelea hususani inabaisha jinsi wanavyojumuishwa katika uchumi wa kimataifa. Wakulima hao ni waathirika wa mabadiliko ya tabianchi , lakini pia ni watu muhimu katika kufikia njia ya maendeleo yanayojali mazingira imesema ripoti.

Pia imetaka hatua za kitaifa, kikanda na kimataifa ikiwemo biashara ya kimataifa na mikataba ya uwekezaji kuhakikisha vinatoa fursa ya biashara kwa wakulima wadogowadogo, ili kufikia ajenda ya mwaka 2030 ya maendeleo endelevu ripoti inasema mambo kufanyika kama yalivyozoeleka sio chaguo.