Skip to main content

Zaidi ya watoto milioni 16 wamezaliwa kwenye vita mwaka huu:UNICEF

Zaidi ya watoto milioni 16 wamezaliwa kwenye vita mwaka huu:UNICEF

Zaidi ya watoto milioni 16 wamezaliwa katika maeneo yenye vita mwaka huu wa 2015 , ikiwa ni mtoto mmoja kati ya wanane waliozaliwa duniani kote . Joseph Msami na taarifa kamili.

Hii ni kwa mujibu wa takwimu za shirika la Umoja wa matyaifa la kuhudumia watoto UNICEF ambazo zinaainisha madhila yanayowakabili watoto kila uchao ambao wanazaliwa katika mazingira magumu kama anavyofafanua  Christophe Boulerac msemaji wa UNICEF

(SAUTI YA CHRISTOPHE)

"Kweli ni mchanganiko wa matatizo kwa watoto hao ambao wanazaliwa kila sekunde mbili. Kwa nini? tuanze na mama zao, hakuna usaidizi wa afya wanapojifungua, wala kwa watoto. Tunapaswa kutambua kwamba hatari hizo zinaongezeka kwa watoto hao, na wakikua watapata shida ya chakula, shida ya kwenda shule na huduma za msingi za afya"

Zaidi ya watoto 200,000 wamearifiwa kuomba ukimbizi Muungano wa Ulaya katika miezi tisa ya mwanzo mwaka 2015 , huku  wengine milioni 30 walilazimika kukimbia makwao 2014 kutokana na vita.