Skip to main content

Licha ya kupungua kwa mashambulizi damu bado inamwagika Mashariki ya Kati: Jenca

Licha ya kupungua kwa mashambulizi damu bado inamwagika Mashariki ya Kati: Jenca

Baraza la usalama la Umoja wa mataifa leo limejadili hali ya Mashariki ya Kati likiwemo suala Wapalestina. Akitia taarifa kwenye baraza hilo kuhusu hali Israel na Palestina , msaidizi wa Katibu mkuu wa masuala ya kisiasa Miroslav Jenca amesema, licha ya kupungua kwa mashambulizi katika wiki chache zilizopita , umwagikaji wa damu haujakoma, huku waisrael 7 na Wapalestina 34 wakiuawa katika wiki hizo.

Amesema kuchoma visu, kushambulia magari na kuua kwa risasi kunakofanywa na Wapalestina kukiwalenga Waisrael bado kunaendelea kukatili maisha ya watu kila siku, huku mapambano yanayoendelea yanasabbisha vifo kwa Wapalestina pia. Amesitaka pande zote kuchukua hatua kukomesha vifo hivyo

(SAUTI YA JENCA)

Ili kukabili tatizo la leo kwa Israel na Palestina tunahitaji mtazamo thabiti kwa uongozi wa Israel na Palestina kuona mbali Zaidi ya mapigano na kuchukua hatua madhubuti kuunda mustakhbali wenye Amani.” Natoa wito kwao kuachana na hofu zao za kisiasa na kujikita katika kufikia Amani ya kudumu kwa watu wa Palestina na Israel”

Ameongeza kuwa Umoja wa mataifa umesimama kidete kuendelea kuunga mkono juhudi hizo kwa kila hali.