Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi zilizoendelea bado zinatawala katika kueneza utamaduni wao- ripoti ya UNESCO

Nchi zilizoendelea bado zinatawala katika kueneza utamaduni wao- ripoti ya UNESCO

Ripoti mpya ya Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, imebainisha kuwa nchi zilizoendelea kiviwanda bado zimetawala katika kueneza utamaduni wao, licha ya kupitishwa agano la kuendeleza usawa katika kuzalisha na kueneza bidhaa za kitamaduni kutoka nchi zinazoendelea miaka kumi iliyopita. Taarifa kamili na Joshua Mmali

(Taarifa ya Joshua)

Agano la UNESCO kuhusu kulinda na kuendeleza tamaduni mbali mbali lilipitishwa mnamo mwaka 2005, na kuanza kutekelezwa mwaka 2007, likiwa limeridhiwa na nchi 141 na Muungano wa Ulaya kufikia sasa.

Ingawa lililenga kuendeleza utamaduni na bidhaa za kitamaduni kutoka nchi zinazoendelea, ripoti ya UNESCO inayotathmini ufanisi wa agano hilo inaonyesha kuwa bado hali haijabadilika, nchi zilizoendelea zikiwa bado zinatawala katika kueneza bidhaa zao za kitamaduni na utamaduni wao.

Hata hivyo, ripoti inaonyesha jinsi teknolojia inavyotoa fursa kwa sauti mbali mbali kusikika katika mitandao ya habari ya kijamii, ikitoa mfano wa jinsi kuibuka wanahabari wa kiraia na watunga filamu wasio na mafunzo ya kitaaluma kunavyobadilisha fani ya uanahabari.