Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi kubwa ya wafanyakazi wa ndani wahamiaji ni wanawake: ILO

Idadi kubwa ya wafanyakazi wa ndani wahamiaji ni wanawake: ILO

Utafiti mpya wa shirika la kazi duniani, ILO ulioangazia umebaini kuwa zaidi ya asilimia 72 ya wahamiaji Milioni 232 duniani ni wafanya kazi.

Ukipatiwa jina makadirio ya wafanyakazi wahamiaji na wahamiaji wafanyao kazi za ndani, utafiti huo umeonyesha kuwa zaidi ya asilimia 73 ya wafanyakazi hao wa ndani ni wanawake sekta ambayo bado sheria zake haziwapatii haki stahili  na hivyo kuwawake katika mazingira magumu.

Akizungumzia utafiti huo Mkurugenzi mkuu wa ILo Guy Rider amesema utafiti huo ni mchango muhimu wa ILO katika kusaidia utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu, SDGs, hususan lengo namba Nane la kulinda wafanyakazi wakiwemo wahamiaji.

ILO imesema kadri idadi ya wazee inavyoongezeka, wafanyakazi wa ndani watazidi kuhitajika ughaibuni ili kukidhi mahitaji ya utoaji huduma kwenye kaya.

Kwa mantiki hiyo ILO imesema ripoti hii imeonyesha kuwa dunia itahitaji takwimu zaidi kuhusu mwelekeo wa wahamiaji wafanyakazi ili watunga sera waweze kuibuka na sera thabiti.