Skip to main content

Mjadala kuhusu kuelewa na kushughulikia suala la makazi unafanyika Geneva:UNHCR

Mjadala kuhusu kuelewa na kushughulikia suala la makazi unafanyika Geneva:UNHCR

Kamishina mkuu wa shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR bwana Antonio Guterres amesema dunia hivi sasa ipo njia panda kwa mtazamo wa kibinadamu inakabiliwa na mambo mawili makubwa: vita, tatizo la usalama kimataifa , lakini pili ongezeko la majanga ya asili na mabadiliko ya tabianchi ambavyo vipo na vitaendelea kusakama mustakhbali wetu. Flora Nducha na taarifa Zaidi.

(TAARIFA YA FLORA NDUCHA)

Akizungumza katika ufunguzi wa mjadala wa kuelewa na kushughulikia suala la makazi  mjini Geneva Bwana Guterres amesema katika miaka ya karibuni dunia imeshuhudia mamilioni ya watu wakilazimika kukimbia makazi yao kutokana na vita na majanga ya asili, huku idadi ya wakimbizi vita ikiwa mara tatu mwaka 2010 na 2014 , wakati muongo uliopita ukielewa kuwa miaka mitatu ya joto la kupindukia.Amesema matatizo haya mawili ya mabadiliko ya tabia nchi na vita yanatanabaisha umuhimu wa uongozi wa kisiasa na utawala bora.

(SAUTI YA ANTONIO GUTERRES)

Ukweli kwamba tunashuhudia kuzuka kwa migogoro mipya mingi kabla ya awali kutatuliwa inaonyesha uhahiri ukosefu wa uwezo na utashi wa kisiasa wa kumaliza vita ukiachia mbali kuvizuia .Kwa upande mwingine baada ya miaka mingi ya majadiliano, makubaliano ya kihistoria ya Jumamosi iliyopita kuhusu mabadiliko ya tabia nchi ni ishara ya hatua kubwa ya mabadiliko ya jinsi dunia inavyokabiliana na moja ya matatizo magumu yanayotukabili leo”

Vita na mabadiliko ya tabianchi ni miongoni mwa sababu kubwa zinazoongoza kwa watu kukimbia makwao.