Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM bado una matumaini ya mchakato wa kisiasa Sahara Magharibi:

UM bado una matumaini ya mchakato wa kisiasa Sahara Magharibi:

Umoja wa Mataifa unasalia na matumaini kwamba mchakato wa kisiasa unaweza kusonga mbele Sahara Magharibi karibu miaka 25 baada ya ujumbe wa kulinda amani kuidhinishwa eneo hilo.

Sahara Magharibi ilikuwa chini ya uongozi wa Hispania hadi mwaka 1976 ambapo nchi jirani zikadai umiliki wake ambazo ni Morocco and Mauritania.

Mpango wa Umoja wa mataifa wa Sahara Maharibi (MINURSO) ulianzishwa mwaka 1991 ili kulinda Amani katika eneo hilo. Kim Boulduc ni mkuu wa MINURSO na karibuni ametoa taarifa kwenye baraza la usalama kuhusu hali Sahara Magharibi

(SAUTI YA KIM BOULDUC)

"Na nadhani ni muhimu sana kutambua mchango wa miaka mingi wa MINURSO, mchango ambao mara nyingi haijulikani. Naweza kusema kwa muhtasari ni ujumbe ndogo unaohudumia eneo kubwa la jangwa la Sahara. Kwa hiyo mazingira ya kazi ni magumu mno . Aidha nyakati za sasa tunajihusisha na mchakato wa kisiasa ambao unaongozwa na mjumbe maalum."