Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP yaanza uzalishaji wa vipande vya tende kwa ajili ya lishe mashuleni Syria

WFP yaanza uzalishaji wa vipande vya tende kwa ajili ya lishe mashuleni Syria

Shirika la Umoja wa mataifa la mpango wa chakula WFP limeanza uzalishaji wa vipande vya tende vilivyoongezewa vitamini na virutubisho vingine nchini Syria kama sehemu ya mpango wake wa kuwalisha watoto takribani 315,000 mashuleni.

Mradi huo wa uzalishaji unaosaidiwa na Muungano wa Ulaya , unasaidia kuwafanya watoto wakae madarasani , ukiwekeza katika mustakhbali wao na wakati huohuo unainua uwezo wa uzalishaji wa chakula katika jamii ambao unatoa ajira na vilevile kuchagiza ukuaji wa uchumi.

WFP imeongeza kuwa mradi wa ulishaji watoto mashuleni nchini Syria unasaidia kuhakikisha kwamba watoto wan chi hiyo wanapata msaada wa lishe inayohitajika kukabiliana na athari za machafuko, lakini pia kurejesha hali ya kawaida kwa maelfu ya familia.

WFP ilianza mradi wa kulisha watoto mashuleni 2014 ikishirikina na UNICEF na wizara ya elimu ya Syria na inampango wa kupanua wigo wa mradi huo mwaka 2016 na kufikia watoto 500,000