Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ripoti ya maendeleo ya binadamu yapambanua kile kinachopaswa kufanyika:UNDP

Ripoti ya maendeleo ya binadamu yapambanua kile kinachopaswa kufanyika:UNDP

Hii leo imezinduliwa ripoti mpya kuhusu maendeleo ya binadamu ikitanabaisha yale yanayopaswa kuzingatia ili fursa zitokanazo na maendeleo ya teknolojia ziweze kuwa na manufaa kwa wote pindi linapokuja suala la ajira na maendeleo endelevu. Mathalani ripoti hiyo iliyoandaliwa na shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa, UNDP, inasema kuwa maendeleo ya teknolojia yamerahisisha utendaji kazi lakini wanufaika ni wachache, wanawake nao wakiwa wahanga zaidi kwani kile wanachofanya kinakuwa nje ya mfumo rasmi wa ajira kinakuwa hakihesabiwi na hata hakitambuliwi. Je kwa Afrika ripoti hiyo ina maana gani? Amina Hassan wa Idhaa hii amezungumza na James Wakiaga, mshauri mwandamizi wa UNDP, Ethiopia na anaanza kwa kufafanua.