Skip to main content

Luteni Jenerali Kamanzi wa Rwanda kuongoza UNAMID

Luteni Jenerali Kamanzi wa Rwanda kuongoza UNAMID

Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika umemteua Luteni Jenerali Frank Mushyo Kamanzi wa Rwanda kuwa kamanda mkuu wa kikosi chao cha pamoja huko Darfur, UNAMID.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa katika taarifa yake amesema uteuzi huo umetangazwa na Katibu Mkuu Ban Ki-moon na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Muungano wa Afrika, Nkosazana Dlamini Zuma.

Luteni Jenerali Kamanzi anachukua nafasi ya Luteni Jenerali Paul Mella wa Tanzania ambaye anamaliza muda wake tarehe 31 mwezi huu ambapo Umoja wa Mataifa umeshukuru kwa utendaji wake wa kujitoa kwa dhati wakati wa uongozi wake.

Kamanda Mkuu wa UNAMID, Luteni Jenerali Kamanzi ameshika nyadhifa mbali mbali ikiwemo mnadhimu mkuu wa jeshi la Rwanda na naibu kamanda mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Afrika huko Sudan kati yam waka 2006-2007.