Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkataba wa Paris ni kiashiria nchi ziko tayari: Pasztor

Mkataba wa Paris ni kiashiria nchi ziko tayari: Pasztor

Msaidizi wa katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya tabianchi, Janos Pasztor amezungumzia kupitishwa kwa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi huko Paris, Ufaransa akisema jambo la msingi nchi zimeamua kuchukua hatua kukabiliana na hali hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini NewYork, Marekani, Bwana Pasztor amesema hakuna pingamizi lolote lililotokea licha ya maoni ya mambo ya kuzingatia baada ya kupitishwa kwa mkataba huo.

(Sauti ya Pasztor)

“Kila nchi, kila makundi ya nchi yaliweza kuwa na kitu cha kurejea nacho nyumbani, jambo muhimu kwao na hilo ndilo jambo chanya. Na kama ilivyo kwa mkataba wowote, jambo la msingi ni kwamba kuna mkataba na hakuna pingamizi lolote lililowekwa. Na hakukuwepo na pingamizi lolote lililowekwa."

Mkataba huo mpya pamoja na mambo mengine unatambua kwamba mabadiliko ya tabia nchi ni tishio kubwa kwa binadamu na jamii zao na hivyo dunia inahitaji ushirikiano na ushiriki wa kila mmoja katika kukabiliana na kupunguza gesi ya viwandani.