Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF/ WFP kusaidia watoto Syria na Jordan msimu wa baridi

UNICEF/ WFP kusaidia watoto Syria na Jordan msimu wa baridi

Wakati msimu wa baridi kali ukinyemelea nchini Jordan , shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na lile la mpango wa chakula duniani WFP wamezindua mpango wa msaada wa fedha  kwa ajili ya msimu wa baridi , msaada ambao utazisaidia familia za Syria zilizoko katika kambi za Za’atari na Azraq kununua mavazi ya kjikinga na baridi kwa ajili ya watoto wao.

Huu ni mwaka wa pili kwa UNICEF na WFP kushirikiana kutoa msaada kwa ajili ya watoto wa Syria wakati wa  msimu wa baridi. Msaada huo wa mara moja kutoka UNICEF utatoa Dinara 20 za Jordan kwa kila mtoto kwa jumla ya watoto 51,851 waio na umri wa chini ya miaka 18 katika kambi hizo mbili.

Msaada huo utawasilishwa kwa njia ya vocha za chakula zilizotolewa na WFP kwa familia hizo kununua chakula kila mwezi. Fedha hizo zitatumika kununu mahitaji ya msimu wa baridi kama buti, suruali, makoti, glavu za kuvaa mikononi na hijab kwenye duka linalosimamiwa na WFP kwenye kambi hizo.