Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

O’Brien ahitimisha ziara Syria

O’Brien ahitimisha ziara Syria

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA bwana Sthephen O’Brien amekuwa ziarani nchini Syria tangu Desemba 12 na ziara hiyo inahitimishwa leo desemba 14.

Lengo la ziara yake ni kutathimini  shughuli za kbinadamu na kujionea mwenyewe athari za mapigano na operesheni za kijeshi kwa raia. Wakati mgogoro huo ukiingia mwaka wa tano mzaidi ya watu milioni 13.5 wanahitaji ulinzi na mahitaji ya lazima.

Watu hao wanakabiliwa na ukatili huku familia nne kati ya tano nchini Syria sasa zinaishi katika umasikini  huku wengine mamilioni hawana chakula cha kutosha, maji safi na malazi.

Wakati wa ziara yake bwana O’Brien alitarajiwa kukutana na familia za wakimbizi, maafisa wa serikali, mashirika ya misaada ya kibinadamu na wadau wengine ili kujadili njia za kuimarisha fursa za kuwafikia maelfu ya watu wanaohitaji msaada ili kuokoa maisha yao.