Skip to main content

Ban atoa wito wa kura ya maoni CAR kufanyika kwa Amani na utulivu:

Ban atoa wito wa kura ya maoni CAR kufanyika kwa Amani na utulivu:

Katika mkesha wa kura yya maoni ya mswada wa katika nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ametoa wito kwa wadau wote kuhakikisha kwamba kura hiyo inafanyika kwa  amani, utulivu na inavyostahili.

Kura hiyo ya maoni ni hatua muhimu kuelekea kumaliza kwa kipindi cha mpito nchini CAR ambayo itaweka mwelekeo na msingi wa mstakhbali wan chi hiyo na watu wake.

Katibu Mkuu amerejea msimamo kwamba Umoja wa Mataifa utaendelea kusaidia juhudi za serikali ya mpito CAR na mchakato wa uchaguzi.