Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ni fursa ya kihistoria kupitisha mkataba wa COP21: Ban

Ni fursa ya kihistoria kupitisha mkataba wa COP21: Ban

Kufuatia kupitisha kwa mkataba mpya wa mabadiliko ya tabia nchi mjini Paris hii leo, Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-Moon amesema wawakilishi wa serikali wameandika historia.Amesema pande husika zimekubaliana katika vipengee vyote muhimu.

(SAUTI YA  BAN KI-MOON)

"Ni kabambe, rahisi,  wa kuaminika na wa muda mrefu. Nchi zote walikubaliana kupunguza kimataifa kupanda kwa joto kwa nyuzi chini ya 2 Celsius. Kwa kutambua hatari na Madhara makubwa, Walikubaliana pia Kuendeleza Jitihada za kudhibiti Ongezeko la joto kwa nyuzi 1.5 C. Hii ni muhimu hasa kwa mataifa ya Afrika, mataifa ya visiwa vidogo nan chi  zinazoendelea.  Umeisikiliza sauti za walio katika mazingira magumu na kutambuliwa umuhimu wa kupunguza na kukabiliana na hasara na uharibifu. "

Ameongeza kuwa Mkataba wa Paris ni ushindi mkubwa kwa watu na dunia yetu, unaweka mazingira ya hatua kwa hatua katika kukomesha umaskini, kuimarisha amani na Kuhakikisha maisha ya hadhi na fursa kwa wote."

Kwa mara ya kwanza wanachama 195 wa mpango wa mkataba wa Umoja wa mataifa wa mabadiliko ya tabia nchi UNFCCC wameahidi kupunguza gesi inayochafua mazingira, kuimarisha vita dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi, na kuchukua msimamo wa hatua za pamoja.

Hatua hiyo inafuatia wiki mbili za majadiliano kwenye mkutano wa Umoja wa mataifa wa mabadiliko ya tabia nchi COP21 .