Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatimaye Mkataba wa mabadiliko ya tabia nchi wapitishwa COP21

Hatimaye Mkataba wa mabadiliko ya tabia nchi wapitishwa COP21

Baada ya vuta nikuvute na ngojangoja ya majuma mawili mkataba mpya wa mabadiliko ya tabia nchi hatimaye umepitishwa baada ya kutathiminiwa na kuidhinishwa na pande zote husika shangwe na nderemo zikatawala

(SAUTI MAKOFI NA VIGELEGELE)

Mkataba mpya unatambua kwamba mabadiliko ya tabia nchi ni tishio kubwa binadamu na jamii zao na hivyo dunia inahitaji ushirikiano na ushiriki wa kila mmoja katika kukabiliana na kupunguza gesi ya viwandani.

Pia unatambua kwamba kupunguza kwa kiasi kikubwa gesi ya viwandani kunahitajika ili kufikia malengo ya kupambana na mabadiliko ya tabia nchi.

Mkataba umeafiki kuchagiza ushirikiano wa kikanda na kimataifa ili kuwepo na malengo imara Zaidi ya kukabili mabadiliko ya tabia nchi  kwa hatua kuchukuliwa na pande zote  na zile zisozohusika zikiwemo asasi za kijamii, sekta binafsi, taasisi za kifedha, miji, uongozi wa jumuiya za kijamii, na jamii za watu wa asili.

Hata hivyo wadau kwenye mkutano huo wamekuwa na maoni mbalimbali kuhusu mkataba mpya uliopitishwa. Kwa niaba ya Afrika Judy Wakhungu,waziri wa mazingira wa Kenya anasema Afrika imeridhika japo sio kila walilotarajiwa limejumuishwa lakini kwa asilimia 80 umekidhi matakwa yao na kilichosalia sasa ni kuanza utekelezaji

(SAUTI YA JUDITH WAKHUNGU)

Naye Richard S Muyungi mkuu wa majadiliano kitengo cha mazingira kutoka ofisi ya Makamu wa Rais nchini Tanzania anasema japo mkataba sio mzuri sana lakini sio mbaya sana hivyo ni siku muhimu

(MUYUNGI CUT 1)

Akasema baada ya safari ndefu kupitishwa kwa mkataba wa leo ni ushindi kwa dunia nzima.

(MUYUNGI CUT2)