Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ameipongeza Saudia kuendesha mkutano wa wapinzani wa Syria:

Ban ameipongeza Saudia kuendesha mkutano wa wapinzani wa Syria:

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon ameipongeza Saudi Arabia kwa juhudi na uongozi wake katika kuendesha mkutano wa upande wa upinzani wa Syria uliofanyika mjini Riyadh kati ya Desemba  9-10.

Katibu Mkuu ameainisha umuhimu wa kuendelea na juhudi za mtazamo chanya wa kundi la kimataifa la uungaji mkono Syria ISSG, ambazo zinaliruhusu kundi hilo kusonga mbele na kuanzisha majadiliano muhimu ya kisiasa mionini mwa Wasyria yalianza mwezi Januari.

Majadiliano hayo yanalengo la kutekeleza azimio la 2012 la Geneva na matamko ya ISSG ya Vienna.