Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama limelaani vikali shambulio la Kabul

Baraza la Usalama limelaani vikali shambulio la Kabul

Wajumbe wa baraza la usalama wamelaani vikali shambulio la jana kwenye ubalozi wa Hispania mjini Kabul ambalo limesababisha vifo vya watu wawili, polisi raia wa Afghanistan na afisa wa jeshi la polisi la Hispania aliyekuwa akifanya kazi kwenye ubalozi huo. Pia watu wengine kadhaa wamejeruhiwa kwenye shambulio hilo ambalo kundi la Taliban limedai kuhusika.

Wajumbe wa baraza wameelezea masikitiko yao na kutuma salamu za rambirambi kwa familia za walioathirika na shambulio hilo, ikiwemo serikali ya Afghanistan na Hispania.

Wajumbe hao pia wamerejea kuelezea hofu yao juu ya tishio kwa umma, majeshi ya serikali na uwepo wa kimataifa nchini Afghanistan , tishio litokanalo na wanamgambo wa Taliban, Al-Qaida, ISIL na wafuasi wao na makundi mengine yenye silaha yanayoendesha harakati zao kinyemela.