Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakati wa kujua mbivu na mbichi umewadia COP21:

Wakati wa kujua mbivu na mbichi umewadia COP21:

Wakati wa kujua mbivu na mbichi umewadia kwenye mkutano wa COP21 unaoendelea mjini Paris Ufaransa. Hiyo ni kauli ya Rais wa COP21 Laurent Fabius mbele ya jopo la wawakilishi waliokusanyika kwenye majadiliano ya tabia nchi kabla ya kutolewa mswada wa mwisho wa muafaka wa mkutano huo kuhusu mabadiliko ya tabia nchi.

Bwana Fabius amesistiza kwamba haya ni makubaliano ambayo pande zote zitaweza kwenda nayo nyumbani wakiwa kifua mbele. Naye Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon mameuambia ujumbe huo kwamba dunia imepewa rasimu ya kihistoria ambayo inaahidi kuweka njia mpya ya kupunguza uzalishaji wa hewa chafu ,a mustakhbali imara wa tabia nchi siku za usoni.

Rasimu hiyo ya muafaka wa mwisho wa mabadiliko ya tabia nchi imekabidhiwa kwa nchi wanachama kuifanyia tathimini, ambapo Ban ametoa wito kwa pande zote kukamilisha kazi waliyoianza

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

"Mwisho unanyatia. Hebu sasa tumalize kazi. Dunia nzima inatuangalia. Mabilioni ya watu wanategemea hekima yako, "

Ameongeza kuwa anataji kuungna na wajumbe wote baadaye kusherehekea muafaka mpya.

Na katika hotuba ya hamasa iliyoambatana na machozi na shangwe waziri Laurent Fabius amewaambia wajumbe rasimu ya sasa ina vipengee vinavyozingatia matakwa ya kikanda.Ili mkataba huo mpya wa kimataifa wa mabadiliko ya tabia nchi uanze kufanya kazi utahitaji pande zote 196 wanachama wa mpango wa mkataba wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabia nchi UNFCCC kupitisha rasimu hiyo.