Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku ya kimataifa ya milima, dunia itambue umuhimu wake katika uchumi

Siku ya kimataifa ya milima, dunia itambue umuhimu wake katika uchumi

Leo ikiwa siku ya kimataifa ya milima, yenye kauli mbiu: "kukuza mazao ya milima kwa ustawi bora", dunia imetakiwa kuthamini uwepo wa rasilimali hiyo ambayo ni kichocheo cha ukuaji endelevu wa uchumi. Joseph Msami na maelezo kamili.

(TAARIFA YA MSAMI)

Katika chapisho lake Umoja wa Mataifa umesema milima sio tu kwamba inasaidia ustawi wa watu zaidi ya milioni 900 duniani kote, lakini pia inawakilisha asilimia 13 ya idadi ya watu, na kunufaisha mabilioni wanaoishi maeneo ya nyanda za chini.

Milima inaelezwa kusaidia kwa kutoa maji safi na asilia, nishati, na chakula ambavyo vinaelezwa kuwa katika karne ziajazo vitakuwa haba.

Licha ya mchango mkubwa ya milima katika ustawi wa jamii, chapisho  hilo linatahadharisha kuwa rasilimali hiyo inakabiliwa na uwezekano mkubwa wa kusababisha umasikini, hatari ya kuathiriwa na mabadiliko ya tabia nchi na ukosefu wa misitu na mmonyoko wa udongo.

Hivyo limeshauri kuanisha fursa endelevu ambazo zaweza kuleta manufaa kwa jamii zote za nyanda za juu na zile za chini ili kusaidia katika kupunguza umasikini bila kuchangia uharibifu wa mazingira.