Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dkt. Posi azungumzia uteuzi wake kwenye Baraza la Mawaziri TZ

Dkt. Posi azungumzia uteuzi wake kwenye Baraza la Mawaziri TZ

Mmoja wa Naibu mawaziri katika baraza jipya la mawaziri lililotangazwa Alhamisi na Rais John Magufuli wa Tanzania, Dkt. Abdallah Pos-i amezungumzia uteuzi huo akisema hakutarajia lakini inaonyesha vile ambavyo watu wana imani na utendaji wake.

Dkt. Posi ambaye ni mlemavu wa ngozi, Albino ameteuliwa kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na walemavu, ambapo ameieleza Idhaa hii kuwa..

(sauti ya Dkt. Posi)

Dkt. Posi akaelezea kile kinachompatia moyo kuweza kusonga mbele licha ya changamoto wanazopata watu wenye ulemavu wa ngozi hususan Tanzania ambako matukio ya mauaji  yamekuwa yakiripotiwa.

(Sauti ya Dkt. Posi)

Kitaaluma, Dokta Posi ni mwanasheria na hadi anateuliwa alikuwa Mhadhiri katika Chuo Kikuu Dodoma na pia ni wakili wa kujitegemea.

Baraza hilo la mawaziri lina wizara 18 ambapo Mawaziri ni 19 na Naibu Mawaziri 16.

Naibu Waziri Mteule Dkt. Posi na mawaziri na naibu mawaziri wengine wataapisha Jumamosi tarehe 12 mwezi huu wa Disemba.