Skip to main content

Jeshi la polisi Tanzania na UN-Women wazindua dawati la jinsia

Jeshi la polisi Tanzania na UN-Women wazindua dawati la jinsia

Tarehe  Saba Disemba wakazi wa eneo la Sitakishari, manispaa ya Ilala jijini Dar es salaam walipata dawati jipya la jinsia na watoto la Jeshi la Polisi katika Kituo cha Polisi cha Sitakishari. Ufunguzi huo ulikuwa sambamba na maadhimisho ya siku 16 za kutokomeza ukatili wa kijinsia ambayo huanza tarehe 25 Novemba hadi tarehe 10 Disemba. Uzinduzi huo umefanyika wakati takwimu zinaonyesha kuwa msichana mmoja kati ya watatu na mvulana mmoja kati ya Saba aliwahil kukumbwa na ukatili wa kingono na zaidi ya asilimia 70 ya wasichana na wavulana waliwahi kusumbuliwa na ukatili wa kimwili kabla hawajafikisha umri wa miaka 18. Je nini kilifanyika? Assumpta Massoi anasimulia zaidi.