Skip to main content

Ni heshima kubwa IOC kuutunukia UM kombe la olimpiki:Ban

Ni heshima kubwa IOC kuutunukia UM kombe la olimpiki:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema amehisi heshima kubwa baada ya kubaini kwamba kamati ya kimataifa ya Olimpiki IOC kuutunuku Umoja wa Mataifa Kombe la Olimpiki. Na kusema yu radhi kulipokea kwa niaba ya Shirika.

Katibu Mkuu anaona tuzohiyo ni ishara ya ushirikiano wa karibu kati ya taasisi hizo mbili. Ameongeza kuwa ushirikiano wetu unatokana na misingi ya maadili na lengo la pamoja la kutumia nguvu ya michezo katika kuchagiza na  kukuza maendeleo na amani.

Katibu Mkuu ameishukuru Kamati ya Olimpiki na Rais wake, Dk Thomas Bach, kwa dhamira yao imara kwa ajili ya Agendaya mwaka 2030 ya maendeleo endelevu.