Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAMA imelaani vikali shambulio katika uwanja wa ndege Kandahar

UNAMA imelaani vikali shambulio katika uwanja wa ndege Kandahar

Mpango wa Umoja wa mataifa nchini Afghanistan UNAMA umelaani vikali shambulio la Taliban kwenye uwanja wa ndege wa Kandahar lililoarifiwa kukatili maisha ya raia 39 wakiwemo watoto wanne na kujeruhi watu wengine 23.

Taliban walifanya shambulio hilo Disemba 8 wakati mapigano yakiendelea kwa saa 24 yaliyolenga maeneo ya raia kwa makusudi walenga raia kwa makusudi.

Taarifa za awali zinaonyesha kwamba wapiganaji wa Taliban waliingia na magari yao kwenye soko na kuanza kufyatua risasi wakiuwa na kujeruhi raia waliokuwa katika manunuzi na wateja wengine.

Mapigano yamearifiwa kuendelea katika maeneo ya makazi ya familia za vikosi vya usalama vya Afghanistan na wafanyakazi wa uwanja wa ndege.