Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Asasi za kiraia zataka makubaliano thabiti kwa sayari salama

Asasi za kiraia zataka makubaliano thabiti kwa sayari salama

Viongozi wa zaidi ya asasi za kiraia 300 kutoka sehemu mbalimbali duniani zinazojihusiaha na masula aya tabiachi leo zimewasilisha saini zaidi ya milioni sita za madai ya hatua stahiki za tabianchi kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.

Katika makabidhiano ya saini hizo kandoni mwa mkutano wa 21 wa mabadiliko ya tabianchi mjini Paris Ufaransa COP 21, asasi hizo zimetaka makubaliano thabiti yatakayoitoa dunia kwenye hewa ukaa na chafuzi na kuipeleka kwenye suluhisho kamilifu. Emma Ruby-Sachs ni Kaimu Mkurugenzi wa asasi iitwayo Abazz.

(SAUTI EMMA)

Akiongea baada ya kukabidhiwa saini hizo Katibu Mkuu Ban Ki-moon amesema

(SAUTI BAN)

Miongoni mwa wanaharakati wanaohudhuria mkutano wa COP 21 ni kikundi cha wafilipino waliotembea kutoka kutoka Vatican hadi Paris.