Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tanzania kuendelea kuchukua hatua dhidi ya ukiukwaji haki:Samia

Tanzania kuendelea kuchukua hatua dhidi ya ukiukwaji haki:Samia

Tanzania imesema licha ya juhudi kubwa ya serikali kuboresha mazingira ya upatikanaji na utoaji wa Haki za Binadamu nchini, bado matukio ya ukiukaji wa haki hizo yameendelea kuongezeka.

Akizungumza jijini Dar es salaam wakati wa siku ya kimataifa ya haki za binadamu, Makamu wa Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amenukuu ripoti na taarifa zinazothibisha uwepo wa matukio kadhaa ya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini.

(Sauti ya Samia)

Kwa upande wake mwenyekiti wa tume ya haki za binadamu nchini humo, Tom Bahame Nyanduga amesemah haki na wajibu ni vitu vinavyoambatana hivyo ametaka kila mtanzania atimize wajibu wake, ikiwa ni pamoja na kuheshimu sheria, ili haki istawi nchini humo.