Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu wengi duniani bado hawajui haki zao:Zeid

Watu wengi duniani bado hawajui haki zao:Zeid

Mwaka huu siku ya haki za binadamu inaadhimisha kuanza kwa kampeni maalumu ya maadhimisho ya miaka 50 ya maagano mawili ya haki za binadamu ambayo ni mkataba wa kimataifa wa haki za kiuchumi, jamii na utamaduni na mkataba wa kimataifa kuhusu haki za kiraia na kisiasa.Grace Kaneiya na taarifa Zaidi

(TAARIFA YA GRACE)

Mikataba hii miwili ni muhimu na inazibana kisheria nchi zilizoiridhia. Katika ujumbe wake wa siku hii Kamishna mkuu wa haki za binadamu

Zeid Ra'ad Al-Hussein amesema, leo hii watu wengi duniani hawajui haki zao au jinsi gani ya kuzitetea.

Na ndio maana ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa mataifa inazindua kampeni ya mwaka mmoja iitwayo “haki zetu, uhuru wetu wakati wote” ikiwa na lengo la kuchagiza kuhusu mikataba ya kimataifa ya haki za binadamu.

Ameongeza kuwa mikataba hii miwili ni msingi kwa kile tunachokiita sheria za kimataifa za haki za binadamu. Hadi sasa kuna mataifa 168 yaliyoridhia mkataba wa kwanza na 164 mkataba wa pili ingali nchi 27 bado hazijaridhia mkataba wowote.