Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkakati wa kimataifa kutokomeza kichaa cha mbwa wazinduliwa:WHO

Mkakati wa kimataifa kutokomeza kichaa cha mbwa wazinduliwa:WHO

Mkakati mpya wa kimataifa wa kutokomeza kichaa cha mbwa kwa binadamu na kuokoa maisha ya maelfu ya watu kila mwaka umezindiliwa leo na shirika la afya duniani WHO kwa ushirikiano na shirika la kimataifa la afya ya mifumo OIE, shirika la chakula na kilimo FAO na muungano wa kimataifa wa kudhibiti kichaa cha mbwa GARC. Flora Nducha na taarifa kamili

(TAARIFA YA FLORA)

Mkakati huo unataka kufanyika kwa mambo matatu muhimu , kwanza kuhakikisha chanjo na kinga nyingine watu wanaweza kumudu, pili kuhakikisha watu wanaoumwa na mbwa wanapata tiba haraka na mwisho kutoa chanjo kwa mbwa ili kukabili kiini cha ugonjwa huo. Margaret Chan ni mkurugenzi mkuu wa WHO

(SAUTI YA MARGARET CHAN)

"Kicha cha mbwa huenda ndio ugonjwa unaouwa zaidi duniani iwapo matibabu hayatolewi kwa wakati muafaka, vifo ni karibu asilimia 100. Ugonjwa wa kichaa cha mbwa unaua makumi ya maelfu ya watu kila mwaka hususan katika maeneo ya vijijini ya Afrika na Asia. Maafa kutokana na ugonjwa huu yanaweza kuzuilika, kichaa cha mbwa kinapaswa kuwa katika vitabu vya historia."

Maelfu ya watu hufa kila mwaka kutokana na kichaa cha mbwa duniani kote huku watu 4 kati ya 10 wanaoumwa na mbwa wanodhaniwa kuwa na kichaa ni watoto wa chini ya miaka 15.