Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Misingi minne ni muhimu kuilinda ili haki iwepo kwa wote:Ban

Misingi minne ni muhimu kuilinda ili haki iwepo kwa wote:Ban

Ikiwa leo ni siku ya haki za binadamu duniani, Katibu Mkuu wa  Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema ni wakati muafaka kuimarisha juhudi za kuendeleza misingi  ya kukabiliana na ukatili unaoenea kila uchao ulimwenguni. Joseph Msami na taarifa zaidi.

(Taarifa ya Msami)

Katika ujumbe wake, Ban amesema ikiwa ni miaka 70 ya Umoja wa Mataifa, dunia inaweza kuchagiza juhudi hizo kwa kuangalia kile ambacho kilifanywa hadi kuibuka kutoka machungu ya vita vikuu vya pili vya dunia.

Kwa mantiki hiyo amesema katika changamoto zinazoikumba duniani hivi sasa, misingi mikuu minne ya uhuru ndiyo inaweza kufanikisha harakati hizo akiitaja kuwa ni uhuru wa kujieleza, uhuru wa kuabudu, mtu kujitosheleza na kutokuwepo na vitisho.

Nchini Tanzania nako maadhimisho ya siku hiyo yamefanyika yakiongozwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye amesema ukiukwaji haki umeendelea mathalani mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi, licha ya juhudi zinazofanywa na serikali, hivyo akasema..

(Sauti Samia)