Rushwa itokomee kwa maendeleo jumuishi: Ban

Rushwa itokomee kwa maendeleo jumuishi: Ban

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kupinga rushwa, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema mitizamo ya dunia kuhusu rushwa inabadilika akitolea mfano kuwa awali rushwa, na fedha haramu ilikuwa kama sehemu ya kufanya biashara sasa ni uhalifu.

Katika ujumbe wake kwa siku hiyo, Ban amesema ajenda 2030 ya maendeleo  endelevu inatambua umuhimu wa kupinga rushwa katika nyanja zote kwani ajenda hiyo inapigia upatu kukomesha umasikini na utu kwa wote.

Ametaka kupungua kwa vitendo vya usafirishaji wa fedha haramu pamoja na urejesho wa mali zilizobiwa akisema kuwa rushwa ina madhara kwa maendeleo kwani fedha ambazo zilipaswa kutumika kwa ajili ya shule, huduma za afya na huduma nyingine muhimu za kijamii huishia kwenye mikono ya wahalifu au maafisa waio waaminifu.

Katibu Mkuu amesema rushwa huchochea uhalifu na ukosefu wa usalama, hufanya taasisi za uma kutotosheka,kupoteza imani ya serikali kwa ujumla pamoja na kuongeza hasira na ukosefu wa utulivu.