Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la usalama lapitisha azimio kuhusu vijana, amani na usalama

Baraza la usalama lapitisha azimio kuhusu vijana, amani na usalama

Kwa mara ya kwanza baraza la usalama leo limepitisha azimio la vijana kuhusu amani na usalama ambalo linatambua mchango wa vijana katika ulinzi na utatuzi wa migogoro. Taarifa zaidi na Amina Hassan

(TAARIFA YA AMINA)

Nats!

Ni kiogozi wa mkutano wa baraza la usalama hii leo balozi David Pressman kutoka Marekani akitangaza kupitishwa kwa azimio hilo llililopitishwa bila kupingwa.

Azimio hilo lililoasisiwa na Jordan na kuungwa mkono na nchi nyingine husuani zile zilizoathiriwa na vitendo vya ugaidi na machafuko kwa ujumla mthalani Nigeria kutoka barani Afrika, linalenga kushughulikia kukuwa kwa misimamo mikali, na makundi kama hayo miongoni mwa vijana.

Akizungumzia azimio hilo la kihistoria katika mahojiano na redio ya UM, mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu vijana Ahmed Alhendawi anasema.

(SAUTI ALHENDAWI)

‘Tumefurahishwa sana na azimio la leo, tunaamini linatuma ujumbe muhimu wa matumaini kwa vijana milioni 600 wanaoshi katika mizozo, linatoa ujumbe wa uhakika kwamba mchango wa kundi hili katika ujenzi wa amani ni muhimu na unapaswa kuungwa mkono. Pia  linatuma ujumbe kwamba ili kuhakikisha amani na usalama tunahitaji kuwekeza kwa kizazi hizi kikubwa cha vijana.’’