Sera mpya za kilimo zizingatie usalama wa chakula:FAO

9 Disemba 2015

Ripoti mpya ya hali ya soko la bidhaa za kilimo imetolewa nashirika la chakula na kilimo FAO. Ripoti hiyo inatoa mapendekezo kuhusu taratibu za biashara ya kimataifa ya chakula na bidhaa za kilimo.

Pia inasema sera mpya zinahitaji kuzingatia kuboresha usalama wa chakula na miradi mingine ya maendeleo, na kuwataka watunga sera kupitia upya sheria za kimataifa za biashara ili kufikia uwiano unaotakiwa. Daniel Gustafson ni naibu mkurugenzi mkuu wa FAO.

(SAUTI YA DANIEL GUSTAFSON)

"Sheria  za biashara zina umuhimu sana katika usimamizi wa biashara ya bidhaa za kilimo na makubaliano hayo yanapaswa kuwezesha nchi kuimarisha usalama wa chakula na lishe bora nchini mwao wakati huo huo kupunguza athari za vitendo vyao kwa nchi zingine"

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter