Hatua zaidi zahitajika kufikia makubaliano COP21: ForumCC

8 Disemba 2015

Wakati majadiliano ya mkataba wa mabadiliko ya tabianchi COP21 yakiendelea mjini Paris Ufaransa, Afrika na masuala ya jinsia yamemulikwa.

Katika mahojiano na idhaa hii Euster Kibona kutoka Tanzania akiwakilisha asasi za kiraia zinazojihusisha na  mabadiliko ya tabianchi, Tanzania Forum CC amesema asasi za kiraia kutoka Afrika zinazoshiriki mkutano huo hazijaridhishwa na hatua za majadiliano kwani maamuzi yasiyo na urari yataathiri bara hilo.

Kuhusu nafasi ya jinsia mwanaharakati huyo amesema

(SAUTI EUSTER)

Kibona pia amesema wanaunga mkono juhudi za Umoja wa Mataifa katika na kwamba madhara ya mabadiliko ya tabia nchi hususani barani Afrika yako dhahiri na huu ni wakati pekee wa kuafikiana.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter