Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dieng atiwa hofu na ukabila Burundi

Dieng atiwa hofu na ukabila Burundi

Dunia ina jukumu la pamoja la kuzuia mauaji ya kimbari ili kuiweka dunia salama amesema mshauri maalum wa Katibu Mkuu kuhusu kuzuia mauaji ya kimbari Adam Dieng.

Akiongea na waandishi wa habari mjini New York kuhusu siku ya kimataifa ya kumbukumbu na utu kwa waathirika wa mauaji ya kimbari na uzuiaji wa uhalifu. Siku hiyo itaadhimishwa kwa mara ya kwanza Desemba tisa hapa UM ambapo Bwan Adieng amesema.

(SAUTI DIENG)

‘‘Kukumbuka matukio ya nyuma, na kutoa heshima kwa wale walioangamia kuimarishe azimio letu la kuzuia matukio kama hayo yasitokee tena kamwe.’’

Akijibu swali kama anaona uwezekanao wa Burundi kuingia katika mauaji ya kimbari amesema

(SAUTI DIENG)

‘‘Ni wakati wa kuchukua hatua. Natiwa hofu sana na matumizi ya ukabila toka pande zote, serikali na upinzani. Historia ya Burundi ni ya machafuko. Kwa kuzingatia kile kilichotokea Rwanda mwaka 1994 , hatuwezi kupuuza umuhimu wa kuchuka hatua mapema’’

Ameonya pia kuwa ikiwa machafuko yanayoendelea Afrika ya kati na Sudan Kusini hayatakomeshwa lolote laweza kutokea.