Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban Ki-moon apongeza wafanyabiashara kwa kushiriki COP21

Ban Ki-moon apongeza wafanyabiashara kwa kushiriki COP21

Zaidi ya viongozi 400 wa sekta ya biashara wamekutana leo mjini Paris Ufaransa kujadili jitihada zao katika kupambana na athari za mabadiliko ya tabianchi, wakati ambapo washiriki wa mkutano wa kimataifa kuhusu tabianchi COP21 wakitarajia kuafikiana kabla ya mwisho wa wiki hii.

Akihutubia kikao hicho, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kwamba ni lazima kubadilisha jinsi ya kufanya biashara zama za sasa ili kuweza kuendelea kufanya biashara siku za usoni,.

(Sauti ya Bwana Ban)

« Duniani kote, wafanya biashara na wawekezaji wameshikamana kwa ajili ya makubaliano thabiti mjini Paris yatakayotuma dalili sahihi kwa soko. Wanatoa ujumbe wa wazi kwamba kutumia vyanzo vya nishati safi na vyenye hewa kidogo ya ukaa kidogo ni lazima, hakukwepeki na kutaleta manufaa »

Amesema sekta zote za jamii zinapaswa kushiriki jitihada hizo, kwani kampuni nyingi zimeshaelewa kwamba zinaweza kuwa fursa ya kiuchumi pia.

Mwaka 2014, zaidi ya kampuni 2,000 zimesajili miradi yao ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kupitia tovuti husika ya Umoja wa Mataifa.