Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la usalama lajadili amani na usalama Afrika

Baraza la usalama lajadili amani na usalama Afrika

Baraza la usalama leo limekuwa na mashauriano kuhusu  amani na usalama barani Afrika ambapo changamoto za usalama katika kanda tofauti barani humo zimeangaziwa ikiwamo ukanda wa Sahel na Afrika Magharibi.

Mwenyekiti wa baraza hilo kwa mwezi huu wa Disemba kutoka Marekani Balozi Samantha Power ameliambia baraza hilo kuwa miongoni mwa suluhu muhimu inayohitaji utekelezaji kwa msaada wa jumuiya ya kimataifa ni kukuza uchumi na kutoa ajira kwa vijana na wanawake.

Baraza la usalama pia limejadili hali nchini jamhuri ya Afrika ya Kati ambapo mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa UM na mkuu wa ofisi ya umoja huo katika ukanda wa Afrika ya Kati UNOCA,  Abdoulaye Bathily amesema vitendo vya uhalifu katika ukanda huo bado ni changamoto kubwa.

(SAUTI ABDOULAYE)

‘Machafuko katika ukanda wetu karibu na bonde la mto Chad, ambao unahusisha misimamo mikali na umasikini sugu wa jamii za pembezoni ni changmoto kubwa. Kumiminika kwa wakimbizi katika bonde hilio kunazidi  uwezo wa serikali na hivyo huduma kufika kimoko kwa maeneo athiriwa.’’

Kikundi cha Lord’s Resistance Army LRA kimetajwa kama tishio la usalama nchini DRC, CAR, na ukanda huo ikijishusisha na biashara ya madini, pembe za ndovu na uhalfu mwingine.