Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mchango wa Jordan kwa wakimbizi wa Syria watambulika UNHCR

Mchango wa Jordan kwa wakimbizi wa Syria watambulika UNHCR

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema linatambua mchango mkubwa wa Jordan kwa kuhifadhi wakimbizi zaidi ya 630,000 wa Syria hali ambayo imeongeza mzigo mkubwa kwa uchumi na miundombinu ya nchi hiyo.

Hata hivyo UNHCR imekuwa na hofu kuhusu wakimbizi 12,000 wanaojaribu kukimbia Syria na kukwama katika maeneo ya vijijini Kaskazini Mashariki mwa mpaka wa Jordan, wakikabiliwa na hali mbaya ya kibinadamu.

Watu hao ni pamoja na 11,000 katika eneo la Rubkan na 1000 katika eneo la Hedalat. Miongoni mwao ni wazee, wagonjwa au majeruhi, watoto, wanawake na wengine wanaohitaji msaada. Idadi ya watu wanaokimbilia maeneo hayo inaendelea kuongezeka tangu Novemba kutoka 4000 na kufikia 12,000 hivi sasa.