Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kutoka MGDs hadi SDGs, WHO yaimarisha utekelezaji wake

Kutoka MGDs hadi SDGs, WHO yaimarisha utekelezaji wake

iliyopita na utafiti kuhusu changamoto za kipindi cha miaka 15 ijayo, ikiangazia malengo ya maendeleo ya milenia MDGs hadi Malengo ya Maendeleo Endelevu SDGs. Grace Kaneiya ya ripoti kamili.

(Taarifa ya Grace)

Kwa mujibu wa ripoti hiyo,  mafanikio yaliyopatikana kwenye MDGs katika kupambana na ukimwi, malaria au vifo vya watoto na wanawake ni kwa sababu ya uwekezaji, ubia na ushiriki wa jamii.

Kuhusu SDGs, ripoti hii imesisistiza umuhimu wa upatikanaji wa huduma za afya kwa wote, ikiwa ni msingi wa kuhakikisha hakuna mtu yeyote anayeachwa nyuma kimaendeleo.

Hata hivyo changamoto kubwa inayoikumba WHO ni ukosefu wa takwimu sahihi kuhusu mifumo ya afya ambayo uimarishaji wake utakuwa kipaumbele cha shirika hilo.

Dk. Ties Boerma ni Mkurugenzi wa Takwimu za afya na mifumo, WHO.

(Sauti Dkt, Ties)

"Juhudi za pamoja zitahitajika zaidi na bima ya afya inawezesha hilo, ushirikiano kati ya sekta mbali mbali utadhihirika zaidi, hivyo si kila sekta kivyake lakini vitu vyote ambavyo vinaathiri binadamu vina uhusiano. Swala hili ni la nchi zote ulimwenguni licha ya kwamba kuna hatari ya maambukizi ya magonjwa au hatari ya maradhi yasiyoambukizwa. Haya ni masuala ya dunia nzima na yanahitaji juhudi za dunia nzima."