Tanzania yataja kiwango cha fedha kinachohitaji kushughulikia na kukabili athari za tabianchi

Tanzania yataja kiwango cha fedha kinachohitaji kushughulikia na kukabili athari za tabianchi

Mkutano wa mabadiliko ya tabianchi ukiendelea huko Paris, Ufaransa, Tanzania imesema inahitaji dola bilioni Moja hadi mwaka 2030 kuhimili na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi nchi, sambamba na dola Bilioni 60 kila mwaka hadi mwaka 2020 kupunguza madhara ya mabadiliko hayo.

Akihutubia kikao cha ngazi ya mawaziri kwenye mkutano huo wa COP21, Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Begum Karim Taj amesema kiwango hicho kitasaidia harakati ambazo tayari  nchi hiyo imeanza kuchukua kukabiliana na mabadiliko hayo, ikiwemo matumizi ya nishati endelevu kama vile gesi asilia na joto ardhi.

Baada ya hotuba hiyo, Balozi Begum alihojiwa na Idhaa hii ambapo amesema pamoja na mahitaji ya fedha hizo suala ni..

(Sauti ya Balozi Begum)