Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wimbi la wakimbizi kutoka Burundi linashuhudiwa kadri mzozo unavyoendelea

Wimbi la wakimbizi kutoka Burundi linashuhudiwa kadri mzozo unavyoendelea

Wakati Umoja wa Mataifa ukiendelea kufuatilia hali nchini Burundi, baadhi ya warundi wanakimbia na kutafuta hifadhi katika nchi jirani kufuatia mzozo wa kisiasa uliogubika nchi hiyo.

Kufuatia hali hiyo wajumbe wa Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wanapanga safari ya kwenda Burundi wakati huu ambapo wameelezwa kuwa serikali ya nchi hiyo haitoi ushirikiano kwa msuluhishi wa Muungano wa Afrika AU na Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC, Rais Yoweri Museveni wa Uganda.

Hali hiyo imesababisha uwepo wa wakimbizi wengi ambao wanakimbia vurugu, mmoja kati ya wakimbizi takribani  laki moja waliokimbilia nchini Tanzania ni Nestor Kamza, basi ungana na Grace Kaneiya katika makala hii kupata mengi