Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ujerumani iwe msitari wa mbele katika kupunguza matumizi ya kemikali zenye sumu:UM

Ujerumani iwe msitari wa mbele katika kupunguza matumizi ya kemikali zenye sumu:UM

Ujerumani iko katika nafasi nzuri ya kuongoza jahazi la kimataifa katika kuzuia athari zitokanazo na matumizi ya kemikali zenye sumu na kukomesha undumila kuwili katika matumizi ya kemikali hizo nje ya Muungano wa Ulaya amesema mtaalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu na hatari ya taka na kemikali Baskut Tuncak

Bwana Tuncak ameyasema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari alipokuwa akiwasilisha matokeo ya awali ya utafiti wake katika hiti isho la ziara yake ya siku nane nchini Ujerumani.

Amesema ukitathimini kupitia haki za binadamu , mafanikio mengi saana nchini Ujerumani na Muungano wa Ulaya yanashaini jambo ambalo limesaidia kulinda na kutambua haki za kupata taarifa, maisha, afya, chakula salama, maji safi ya kunywa, usafi, nyumba bora, mazingira bora na usalama mahali pa kazi.

Ameongeza kuwa lakini kwa bahati mbaya kemikali zilizopigwa marufuku kutumika Muungano wa Ulaya kwa sababu ya athari zake bado zinasafirishwa au kutengenezwa kwa matumizi nje ya mipaka ya Muungano wa Ulaya na makampuni ya Ujerimani na kupelekwa kwa nchi ambazo mifumo yake haziwezi kuhumili athari hizo na hivyo kuwaweka wafanyakazi nan a jamii ya nchi zinazoendelea katika hatari kubwa ya matumizi ya kemikali hizo.