Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ungeni mkono makubaliano ya kisisia Libya: Kobler

Ungeni mkono makubaliano ya kisisia Libya: Kobler

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Libya Martin Kobler, amesisitiza kuwa makubaliano ya kisiasa nchini humo yanalenga kukomesha machafuko katika taifa hilo.

Kobler ambaye pia ni mkuu wa ujumbe wa UM nchini Libya UNSMIL amesema makubaliano hayo ambayo yameungwa mkono na idadi kubwa  ya baraza la kongresi na wabunge ni muhimu kwani nchi hiyo inahitaji amani kufuatia migawanyiko iliyopo sasa.

Amesema huu ni wakati wa kuidhinisha makubalainao hayo akisema kuwa hakuna muda wa kupoteza, huku akitaka pande zote nchini Libya kuunga mkono wakiwamo wale wanaoyapinga.

Katika kuunga mkono makubaliano hayo Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na serikali za Italia na Marekani zitafanya mkutano hivi karibuni wa kutoa msukumo kwa jumuiya ya kimataifa kudhihirisha dhamira ya kuunga mkono makubalinao ya kisiasa ya Libya.