Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakulima wadogowadogo wasiachwe katika suluhu za mabadiliko ya tabianchi: IFAD

Wakulima wadogowadogo wasiachwe katika suluhu za mabadiliko ya tabianchi: IFAD

Ripoti mpya ya mfuko wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo, IFAD inaonyesha kuwa suluhu ya muda mfupi haitoshi kwa wakulima kukabili na kuhimili mabadiliko ya tabia nchi.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo iliyotolewa wakati mkutano kuhusu mabadiliko ya nchi ukiendelea mjini Paris Ufaransa, IFAD inasema ikiwa kuna umuhimu wa kukuza  ustawi wa wakulima wadogowadogo lazima kuhakikisha vipaumbele vyao vinaeleweka na kuakisiwa katika sera.

Kadhalika ripoti hiyo inapendekeza kuwa msaada wa kiufundi mathalani kuongeza mbegu, utabiri sahihi wa hali yua hewa, havitoshi badala yake sera za kitaifa, mikakati ya kisheria na bajeti zitaandaa fursa kwa ajili ya idadi kubwa wanawake na wanaueme vijijini kukabilana na mabadiliko ya tabianchi.