Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF yapanga kuwasaidia watoto milioni 2.6 Syria katika majira ya baridi

UNICEF yapanga kuwasaidia watoto milioni 2.6 Syria katika majira ya baridi

Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limesema msimu mwingine wa baridi kali unanyemelea kwa watoto zaidi ya milioni nane nchini Syria wanaoishi nchini humo au kama wakimbizi katika nchi jirani na kwingineko.

Utabiri wa awali unaashiria kuwa majira ya baridi yatakuwa mabaya zaidi mwaka huu kuliko mwaka jana katika baadhi ya maeneo ya milimani ambako kiwango cha joto kitakuwa chini sana katika jkiezi ya Desemba na Januari.

Kwa mujibu wa Dr Peter Salama ambaye ni mkurugenzi wa kanda ya Mashariki ya Kati na Afrika  wa UNICEF miezi hiyo ni mibaya sana kwa watoto na husasani pale familia zao zinapolazimika kuchoma mipira au vifaa vingine vitoavyo sumu ili kupata joto kwenye makazi yao ya muda.

Vita vinavyoendelea Syria viwewatawanya zaidi ya watoto milioni tatu ndani ya Syria , huku idadi ikiwa hadi mara tatu kwa mataifa jirani ya Uturuki, Lebanon, Jordan ma Misri , ambapo zaidi ya watoto milioni 2.2 wanaishi kama wakimbizi.