Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Somalia kukabiliana na tatizo la mabomu yaliyotegwa ardhini

Somalia kukabiliana na tatizo la mabomu yaliyotegwa ardhini

Serikali ya Somalia kwa ushirikiano na Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na huduma za kung'oa mabomu ya kutegwa ardhini, UNMAS.  imezindua mpango wa kuondoa mabomu yaliyotegwa ardhini na ambayo hayajalipuka.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva Uswisi, Mkuu wa UNMAS nchini humo Alan Macdonald amesema mpango huo ni mzuri na wazi, na UNMAS inasaidia Somalia kusaka ufadhili kwa ajili ya utekelezaji wake na kwamba mpango wa serikali ni kuwezesha serikali za mitaa kubaini mabomu hayo na kuelimisha jamii.

(Sauti ya Macdonald)

Somalia haina shida kubwa ya mabomu yaliyotegwa ardhini na yale ambayo hayajalipuka, lakini inayo kiasi, kutokana na vita vya mpakani na Ethiopia, vita vya Ogaden kwenye miaka ya 70, na pia kutokana na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yanayoendelea kwa miaka 30 sasa, kwa hiyo kuna maeneo kadhaa hatarishi zaidi, ambapo kuna shida ya mabomu yaliyotegwa ardhini ya kukabiliana nayo.”