Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uwiano unahitajika kuepeuka athari za tabianchi kwa kilimo: Dk Nabarro

Uwiano unahitajika kuepeuka athari za tabianchi kwa kilimo: Dk Nabarro

Mkutano wa 21 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi COP21 ukiendelea huko Paris, UFaransa, Mwakilishi maalum wa Katibu  Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu usalama wa chakula na mbadiliko ya tabia nchi Dk David Nabarro amesema ni muhimu kuwa na mizania ya usawa kati ya kilimo na tabianchi kwani vyote viwili vina athari kwa sayari dunia na viumbe vyake. Grace Kaneiya na taarifa kamili.

(Taarifa ya Grace)

Katika mahojiano na redio ya Umoja wa Mataifa wakati wa mkutano huo, Dk Nabarro amesema kuwa athari za mabadiliko hayo kwa kilimo ziko bayana kila kona ya dunia hatua inayoathiri uhakika wa chakula.

Amesema licha ya kwamba kinachoonekana dhahiri kwa wengi ni athari za kilimo zitokanazo na tabianchi lakini kilimo huzalisha hewa chafuzi aina ya  methani ambayo ni chochezi katika kubadili hali ya hewa.

Amesema kilimo kikitumiwa vyema kama vile upandaji wa miti na uhifadhi wa udongo  chaweza kuzuia hewa chafuzi.

Kuhusu athari za usalama wa chakula kutokana na mabadiliko ya tabianchi anasema.

(SAUTI DK NABARRO)

‘‘Tumeshuhudia ongezeko la mara kwa mara la ukame katika ukanda wa Sahel, na pembe ya Afrika na mataifa ambayo ni masikini na ambayo yamekumbwa zaidi za mabadiliko ya tabia nchi. Nina uhakika nikiongea na wakulima wa Afrika na jamii zake, kuna mamilioni ya maisha yaliyoathiriwa na mabadiliko ya tabia nchi.’’